KESHO NI SIKU YA REDIO DUNIANI



Kesho ni maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani.
Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku hiyo mwaka 2018 ni Redio na Michezo.
Maadhimisho ya siku ya Redio Duniani nchini Tanzania yanadhimishwa kitaifa Mkoani Dodoma.
Kauli mbiu ya siku hiyo inalenga kukuza michezo kwa kuzingatia jinsia kupitia Redio.
Maadhimisho hayo yametanguliwa na mafunzo ya waandishi wa habari wa Redio za Jamii nchini Tanzania kuhusu uandaaji wa habari na Vipindi bora, Jinsia na uandishi wa habari za uchunguzi.
Akizungumza na washiriki wa mafunzo hayo, Mkuu wa Ofisi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO, Bi Faith Shayo amewataka waandishi wa habari kuandika habari sahihi na zenye tija kwa jamii.
Mafunzo hayo yameshirikisha waandishi wa habari 49 kutoka vyombo vya habari 24 nchini na yamefadhiliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO.
TAG