JSHI LA ZIMAMOTO LATOA RAI KWA WANANCHI WOTE.

 
Wamiliki wa majengo na vyombo vya usafiri na usafirishaji, wafanyabiashara na wananchi wametakiwa kununua au kufanyia matengenezo vifaa na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto kwa mawakala waliosajiliwa kuuza vifaa vya zimamoto kwa mujibu wa sheria
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limetoa rai hiyo leo Jumatano Januari 3,2018 kupitia taarifa kwa umma iliyotolewa na ofisi ya habari na elimu kwa umma ya Jeshi hilo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Jeshi hilo halifanyi biashara ya kuuza vifaa vya kuzimia moto wala kuvifanyia matengenezo pamoja na mifumo ya kinga na tahadhari dhidi ya moto, bali husimamia na kuhakiki ufungwaji wa vifaa hivyo.

Jeshi hilo lina majukumu ya kuokoa maisha na mali katika majanga yatokanayo na moto, mafuriko, tetemeko la ardhi, ajali za barabarani na majanga mengine.

Pia, linafanya ukaguzi kwenye vyombo vya usafiri na usafirishaji na kutoa ushauri uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari.

Ukaguzi hufanyika kwa mujibu wa sheria namba 14 ya mwaka 2007 ikisomwa pamoja na kanuni ya vyeti na usalama wa moto ya mwaka 2008 na marekebisho ya mwaka 2014 pamoja na kanuni ya tahadhari dhidi ya moto kwenye majengo ya mwaka 2015.
TAG