Wanawake wajawazito wameshauriwa kujenga tabia ya kuhudhuria kliniki pale wanapopata ujauzito ili kuepuka madhara mbalimbali wanayoweza kuyapata ikiwemo kifafa cha mimba.
Ushauri huo
umetolewa leo na dokta Frola Mwinuka
kutoka halmashauri ya mji wa kahama wakati akizungumza katika kipindi cha nondo
kinachorushwa kuanzia jumatatu hadi alhamis kupitia Baloha Fm
Amesema baadhi
ya wanawake wamekuwa wazembe kuhudhuria kliniki mpaka pale wanapo karibia
kujifungua na wasichana wanao beba mimba
katika umri mdogo na hivyo kujiweka katika hatari kubwa ya kupata kifafa cha
mimba.
Dokta Mwinuka pia amebainisha madhara ambayo
anaweza kupata mwanamke endapo atapata kifafa cha mimba na kusisitiza watu
wakaribu na mama mjamzito kuhakikisha wanamuhimiza kuhudhuria kliniki.
Aidha
amesisitiza jamii kutokimbilia dawa za kienyeji kutibu tatizo hilo ama mama
kujifungulia nyumbani na badala yake wamuwahishe katika kituo cha kutolea
huduma za afya.
No comments
Post a Comment