Doug Jones amakuwa mwanasiasa wa
kwanza wa Democrat katika kipindi cha miaka 25 kushinda kiti cha Seneta katika
jimbo la Alabama nchini Marekani baada ya kanpeni kali ya kumpinga mgombea wa
Republican Roy Moore kwa kura 51-49.
Huku asilimia 99 ya kura zikiwa
zimehesabiwa, Bw Moore alikataa kukubali kushindwa Jumanne usiku
Alipambana na kampeni yenye utata
ambapo madai yaliibuka kuhusu dhuluma za kimapenzi na wasichana wadogo.
Bw. Moore ambaye amesema kuwa
anaamini mapenzi ya jinsia moja yanastahili kuharamishwa amekana mara nyingi
madai dhidi yake
Vyombo vingi vya habari vimeripoti
kuwa Jones ameshinda baada ya asilimia 99 ya kura kuhesabiwa.
Lakini Moore, 70 aliwaambia wafuasi
wake kuwa bado mambo hayajakwisha.
Alisema anaamini mwanya wa ushindi
utapungua wakati kura zinaendelea kuhesabiwa.
Licha ya Bw. Moore kukataa
kushindwa, Rais Trump alimpongeza Bw Jones kupitia mtandao wa Twitter muda
mfupi baada ya vyombo vya habari kumtangaza kuwa mshindi.
No comments
Post a Comment