Mikoa miwiliya Shinyanga na Geita imetiliana saini na
kampuni ya ukandarasi ya kutoka China ya Beijing Construction Engeneering
Group kwa ajili ya utekekelezaji wa mradi wa maji unaoanza mapema
mwezi januari mwakani.
Akizungumza kabla ya utiliaji wa saini hiyo ya makubaliano
kati ya tanzania na china mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhil Nkurlu kwa
niaba ya mkuu wa mkoa wa shinyanga,amesema mradi huo mkubwa wa maji utakuwa na
manufaa kwa wananchi wa halmashauri ya Msalala, Shinyanga vijijini
na Nyangh'wale mkoani Geita .
Aidha amewataka wakandarasi hao kukamilisha mradi huo kwa
wakati ama kabla ya muda uliopangwa ili kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo
kuondokana na adha ya maji ya muda mrefu.
Mara baada ya utiliaji wa saini ulio wekwa na mkurugenzi wa
msalala simon berege na mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi Cheng Long
Hai ambapo kwa pamoja wamekamilisha zoezi hilo ili kuanza kwa mradi huo.
Akizungumza mara baada ya zoezi hilo mbunge wa jimbo la
msalala Ezekiel Maige amesema mradi huo umekuwa ni chachu na tumaini
jipya kwa wananchi wa jimbo lake kwani watu wamekuwa wakipata shida ya maji
bila ufumbuzi kwa muda mrefu.
Mradi huo unatarajia kughalimu shilingi bilioni 13.9,
na utatekelezwa kwa miezi kumi na mbili na utakamilika mapema desemba 6 mwakani
.
No comments
Post a Comment