
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewasamehe familia ya mwanamuziki Pappi Nguza Viking ambao walikuwa wamehukumiwa kifungo cha maisha.
Rais
Magufuli ametangaza msamaha huo leo mjini Dodoma kwenye sherehe za Uhuru
wa miaka 56 ya Tanganyika, ambapo pia ametoa msamaha kwa wafungwa 8,157.
“Nimeamua kusamehe
wafungwa 8157, ambapo baada ya msamaha huu, 1828 watatoka leo, 6329
wamepunguziwa muda wa kukaa gerezani”, amesema Rais Magufuli.
Baada ya kutangaza
hivyo rais Magufuli akaongeza kuwa katika msahama huu nimeamua kuisamehe
familia ya Nguza Viking na kuanzia sasa wawe huru kulingana na taratibu za
kimagereza.
Nguza na wanawe
watatu walikamatwa Oktoba 12 mwaka 2003 na walipandishwa kizimbani katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003, wakituhumiwa kubaka na
kunajisi watoto 10, na Juni 25, 2004 Mahakama iliwatia hatiani na
kuwahukumu kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam
No comments
Post a Comment