
Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa chama cha ACT Wazalendo
taifa, ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Anna Elisha Mghwira
ametangaza rasmi kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Mghwira ametangaza uamuzi huo alipokuwa akizungumza
kwenye mkutano wa Umoja wa Wanawake wa Chama cha Mapinduzi (UWT) unaofanyika
mkoani Dodoma.
RC huyo wa Kilimanjaro amesema amefikia uamuzi huo
kutokana na utendaji wa serikali ya awamu ya tano, hivyo ameona ni vyema
ajiunge na CCM ili kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Dkt. John
Pombe Magufuli.
“Nimeiona
CCM inayobadilika, nimeona juhudi za kila mtu, ninaiona CCM inayoanza kukataa
rushwa, nimeiona CCM inayoanza kulipeleka taifa mbele,“ amesema Mghwira kwenye mkutano huo na kuongeza.
“Ninataka
niseme kwamba baada ya kufanya kazi chini ya serikali hii kwa miezi takribani
sita saba sasa ninaona nina sababu ya kutangaza kwamba ninapenda kuungana na
Chama cha Mapinduzi.”
No comments
Post a Comment