Wamiliki wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kutoingilia
uhuru wa wanahabari katika vituo vyao kwa sababu vinaongozwa na sera na misingi
ya taaluma ya habari.
Hayo yamebainishwa mjini DODOMA na Mkufunzi Mwandamizi
wa Radio za kijamii Bi Rose Mwalimu katika warsha ya kuwajengea uwezo waandishi
wa habari vijijini ambayo imewakutanisha wadau wa Redio za jamii nchini.
Amesema ni vyema wanahabari wakawa huru katika kutimiza
wajibu wao kitaaluma ili kuihudumia jamii na kujiepusha na masuala binafsi.
Warsha hiyo ya siku nane imewashirikisha wadau
wa Redio za jamii 24 imeandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu,
Sayansi na Utamaduni, UNESCO ili kuwajengea uwezo waandishi wa habari
kujiendesha kwa kujiamini.
No comments
Post a Comment