TUSEME KUPINGA UKATILI DHIDI YA WATOTO, SHINYANGA.



 Image result for Save the Children, shinyanga waanzisha club
Shirika la Kimataifa la Save the Children kwa kushirikiana na shirika la Rafiki Social Development Organization (SDO)mjini Shinyanga wamefanya mkutano wa ‘Klabu za Tuseme’ kutoka shule 8 za msingi na sekondari kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya klabu hizo katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto.
Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha wanafunzi kutoka shule 8 za msingi na sekondari ambazo ni Ushirika,Mwasele,Solwa,BugoyiA,Lyabusalu,Masekelo, Iselamagazi na Mwantin katika manispaa ya shinyanga na halmashauri ya shinyanga vijijini.
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children Alex Enock amesema klabu za Tuseme zimeundwa kupitia mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawala unaotekelezwa na shirika hilo kwa kushirikiana na Shirika la Rafiki SDO kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la nchini Sweeden (SIDA).
Enock amesema lengo la klabu hizo ni kumsaidia mtoto wa kike kukabiliana na vitendo vya ukatili ikiwemo kupewa ujauzito na kuepuka vishawishi mbalimbali ili aweze kumaliza masomo yake salama.
 Naye afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawala kutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement ameeleza katika kutekeleza mradi huo wameshirikiana na idara ya elimu msingi na sekondari kuanzisha klabu za Tuseme kwa ajili ya kuhamasisha ufaulu hasa kwa watoto wa kike.
Wakizungumza katika mkutano huo,wanafunzi hao wamesema klabu hizo zimewasaidia kwa kiasi kikubwa kujiamini,kuepuka vishawishi mbalimbali lakini pia wamekuwa mabalozi wazuri katika kuielemisha jamii juu ya haki za watoto.
TAG