
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amewasili Mkoani
Dodoma ambako pamoja na mambo mengine atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za
maadhimisho ya miaka 56 ya Uhuru.
Katika Ikulu ya
Chamwino, Rais Magufuli amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt.
Binilith Satano Mahenge.
Akiwa Mkoani
Dodoma Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
atafungua vikao vya Jumuiya za CCM na pia atakuwa mgeni rasmi katika shughuli
mbalimbali za kiserikali.
Mhe. Rais Magufuli
ameongozana na Mkewe Mhe. Mama Janeth Magufuli.
Sherehe za Uhuru
zinatarajiwa kufanyika katika uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi tarehe 09
Desemba, 2017.
No comments
Post a Comment