WAFUGAJI KAHAMA WAPIGWA "STOP" KUHUSU HILI...

Image result for ufugaji wa ng'ombe
Imeelezwa kuwa mfugaji asiyeshiriki katika zoezi la upigaji chapa hataruhusiwa kuuza ama kusafirisha mifugo yake  katika Halmashauri ya mji wa Kahama wilayani humo mkoani Shinyanga.

Akizungumza na Baloha fm Afisa Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya mji wa Kahama Costantine Lugendo amesema zoezi hilo ni muhimu kwa mfugaji  na ni agizo la serikali kuu na linafanyika nchi nzima.

Aidha Lugendo ameiambia Baloha FM kuwa zoezi hilo lina manufaa kwa mfugaji kwani litawezesha utambuzi wa mifugo endapo imepotea.

Hata hivyo Afisa Mifugo huyo amebainisha kuwa zoezi la upigaji chapa lilianza mapema mwezi Machi mwaka huu lakini lilisimama baada ya kuwepo na changamoto ya nyenzo za kufanyia kazi.

Zoezi la upigaji chapa  amefafanua ni endelevu ambapo litakuwa linafanyika mara baada ya miezi kadhaa huku umri wa ng'ombe kuwekewa chapa ni kuanzia umri wa miezi 6.



TAG