JAMII YATAKIWA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA.


Image result for dawati la jinsia


Kufuatia kuanza  siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia jamii imehimizwa kushiriki kupinga vitendo vyote vya kikatili.

Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga  NINAELI KISAGASE wakati akizungumza na Baloha fm.

KISAGASE amesema endapo jamii itashiriki kikamilifu kupaza sauti kutoa taarifa itasaidia watuhumiwa kukamatwa na sheria kuchukua mkondo wake.

Amesema licha ya ukatili wa kijinsia kuendelea lakini jamii imeanza kupata uelewa kuhusu haki zao za msingi  pale zinapovunjwa na kutoa maelezo katika dawati hilo.

Aidha ameeleza  kwa sasa wapo katika siku kumi na sita za kupinga ukatili hivyo jamii  haina budi kutoa taarifa kwa haraka na sio kuyafumbia macho pindi wanapoona matendo ya kikatili yakitendeka.
TAG