JKT RUVU iko kundi A katika ligi hiyo.
Afisa Habari wa Timu hiyo, COSTANTINE MASANJA ameiambia BALOHA FM kuwa JKT RUVU imeingia kambini chini ya Kocha Mkuu, BAKARI SHIME.
MASANJA amesema hatua hiyo inalenga kuiweka timu hiyo katika mazingira bora ikiwa ni kujiandaa kwa michezo ya ligi hiyo ambayo imebaki.
Kwa mujibu wa Ratiba ya Kundi A, Desemba 16, mwaka huu JKT RUVU itacheza na KILUVYA UNITED katika uwanja wa FILBERT BAYI uliopo Mkoani PWANI.
Katika hatua nyingine, Timu ya JKT RUVU haikufanya mabadiliko katika dirisha dogo la usajili.
No comments
Post a Comment