MICHUANO YA CECAFA KUANZA JUMAPILI KENYA



Image result for cecafa logoMichuano ya soka kuwania taji la Afrika Mashariki na Kati CECAFA, inatarajiwa kuanza siku ya Jumapili (Desemba 3, 2017 )nchini Kenya.
Mataifa 10 yatashiriki katika michuano hiyo na tayari droo ya hatua ya makundi imeshatangaza.
Kundi A lina timu za KENYA, RWANDA, LIBYA, TANZANIA na ZANZIBAR wakati Kundi B litakuwa na mataifa ya UGANDA, ZIMBABWE, BURUNDI, ETHIOPIA na SUDAN KUSINI.
Mechi ya ufunguzi itakuwa kati ya wenyeji KENYA na RWANDA lakini mechi nyingine siku hiyo ya kwanza itakuwa ni kati ya LIBYA na TANZANIA.
Michuano hiyo itachezwa katika uwanja wa Bukhungu mjini Kakamega, Afraha Nakuru, Mumias Sports Complex na Moi, mjini Kisumu.
Hata hivyo, kuna wasiwasi michuano hii isifanyika MJINI Kisumu kwa hofu za kiusalama kwa mujibu wa chama cha soka nchini Kenya na sasa uwanja wa Machakos utatumiwa.
Katika Hatua nyingine, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya ZANZIBAR (ZANZIBAR Heroes), HEMED SULEIMAN ‘MOROCCO’ amemuongeza kwenye kikosi kiungo mshambuliaji wa timu ya YANGA, EMANUEL MARTIN ili kuzidi kuipa nguvu timu hiyo itakayokwenda Kenya katika Mashindano ya CECAFA yanayotarajiwa kuanza Desemba 3 hadi 17, 2017.
Katika uteuzi wa awali Martin hakuitwa lakini kocha Morocco amelazimika kumuongeza mshambuliaji huyo na atakuwa mchezaji wa 31 kwenye kikosi cha Heroes kabla ya kuchujwa na kubakia 24 ambao wanatarajia kuondoka Zanzibar kesho Novemba 29, 2017.
Martin ambaye ni mchezaji wa zamani wa JKU ya Zanzibar ataungana na wenzake Ahmed Ali (Taifa ya Jang’ombe), Nassor Mrisho (Okapi), Mohammed Abdulrahman (JKU), Abdallah Haji ‘Ninja’ (Yanga), Mohd Othman Mmanga (Polisi), Ibrahimm Mohammed ‘Sangula’ (Jang’ombe Boys), Adeyum Saleh ‘Machupa’ (Kagera Sugar), Haji Mwinyi Ngwali (Yanga), Abubakar Ame ‘Luiz’ (Mlandege), Issa Haidar ‘Mwalala’ (JKU), Abdulla Kheir ‘Sebo’ (Azam) na Ibrahim Abdallah (Taifa ya Jang’ombe).

Wengine ni Abdul-swamad Kassim (Miembeni City), Abdul Aziz Makame (Taifa ya Jang’ombe),Mudathir Yahya (Singida United), Omar Juma (Chipukizi), Mohd Issa ‘Banka’ (Mtibwa Sugar), Amour Suleiman (JKU), Mbarouk Marshed (Super Falcon), Hamad Mshamata (Chuoni), Suleiman Kassim ‘Selembe’ (Majimaji), Kassim Suleiman (Prisons), Matheo Antony (Yanga), Ali Badru (Taifa ya Jang’ombe), Feisal Salum (JKU), Salum Songoro (KVZ), Khamis Mussa (Jang’ombe boys), Mwalimu Mohd (Jamhuri), Seif Abdallah ‘Karihe’ (Lipuli) na Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto).

TAG