
Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeshauriwa kuanzisha somo la Ukimwi katika shule za Sekondari, ili kuwasaidia wanafunzi kuepukana na ugonjwa huo.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Ikinda Matrida Musoma ,wakati akichangia taarifa ya utekelezaji wa mradi wa kudhibiti Ukimwi kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Msalala kilichofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Amesema taarifa hiyo imebainisha kutekeleza mradi huo kwa kuwapatia elimu vijana ambao hawapo masomoni huku kundi la wanafunzi wa shule za sekondari likisahaulika.
Kutokana na hali hiyo serikali inatakiwa kuanzisha somo la ukimwi katika shule za sekondari ili elimu hiyo iwafikie pia wanafunzi hao.
No comments
Post a Comment