Taasisi mbali mbali zimepigwa marufuku kufanya mikutano ya aina yeyote iwe ya nje ama ndani bila ya kupata kibali , ili kuendelea kudhibiti suala la ulinzi na amani.Kauli hiyo imetolewa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake na kusema kuwa iwapo mikutano hiyo itafanyika hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Aidha amewataka watendaji na viongozi wengine kusimamia zoezi hilo kikamilifu ili kuhakikisha mikutano hiyo haifanyiki bila kuwa na kibali.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ya kahama,amewataka watu wanao uziana nyumba ,viwanja ama makazi ya biashara kuhakikisha wanalipa kodi ya serikali.
Amesema tabia ya kuuziana bila kulipa kodi imekuwa ikifanyika kwa kukwepa kulipa na kuwataka watu kuacha kukwepa kwani atahakikisha kila mmoja atakaeuza analipa bila kukwepa kulipa kodi ya serikali.
No comments
Post a Comment