Klabu ya Celtic imeshtakiwa na shirikisho la soka barani Ulaya Uefa baada ya shabiki mmoja kuingia uwanjani na kujaribu kumpiga teke mshambuliaji wa PSG Kylian Mbappe. Kisa hicho kilitokea katika kipindi cha kwanza cha mtanange huo siku ya Jumanne muda mfupi baada ya wageni hao kuwafunga Celtic bao la tano.
PSG pia inakabiliwa na shtaka la mashabiki wake kuvunja viti vya uwanja huo.
Kesi hiyo itaangaziwa na kitengo cha maadili na nidhamu katika shirikisho la Uefa tarehe19 Octoba.
Kocha wa Celtic Brendan Rodgers amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya mashabiki kumzomea jamaa huyo aliyeingia uwanjani.
Nadhani hatua iliochukuliwa na mashabiki kumzoma jamaa huyo ilikuwa jibu zuri.
Inakatisha tamaa katika uwanja wowote wa klabu yoyote unapoona shabiki anaingia katika uwanja kama alivyofanya.
Takwimu muhimu.
- Celtic's 0-5 loss to Paris Saint-Germain na ni record mpya katika mashindano ya ulaya (UEFA na Europer).
- Marcus Rashford ni mchezaji kinda wa 4 mwingereza kufunga katika UCL kwa Man U akiwa na umri mdogo, wengine ni David Beckham, Wayne Rooney & Phil Jones.
- Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois ni golikipa wa kwanza Champions League ku assist tangu Fraser Forster in Nov 2012.
- Davide Zappacosta ni mchezaji wa 100 wa Italian kufunga katika UCL.
- Kylian Mbappe ni mchezaji pekee kuwahi kutokea kufunga katika UCL akiwa na umri mdogo katika misimu miwili tofauti na klabu mbili tofauti (Monaco & PSG).
- Neymar kashiriki katika mabao 11 (five goals, six assists) katika michezo 5 ya UCL dhidi ya Celtic.
No comments
Post a Comment