VIONGOZI WA ULAYA WAKUTANA NA WENZAO WA AFRIKA MJININI ABIDJAN

 EU-Afrika-Gipfel in Abidjan (picture-alliance/dpa/M. Kappeler)

Viongozi wa Umoja wa ulaya wameanza mazungumzo yao pamoja na viongozi wenzao wa bara la Afrika kuhusu uhamaji, wakipania kuupatia ufumbuzi mzozo wa watu wanaoyatia hatarini maisha yao kwa lengo la kuingia barani Ulaya.

Viongozi kutoka Ufaransa, Ubeigiji, Luxemburg, wote wakiwa ni viongozi wa kiume wenye umri unaokurubia miaka 40 wanajaribu kujitenganisha na picha ya wakoloni wa zamani wa Afrika, wakitetea umuhimu wa kuendeleza biashara na kuwekeza katika miradi ya maendeleo na usalama barani humo pamoja na kushughulikia vyanzo vya uhamaji.
Uhamaji ndio mada kuu katika mkutano huu wa kilele mjini Abidjan, mji mkuu wa kibiashara wa Côte d'Ivoire, mada iliyopata nguvu kutokana na kanda ya video iliyotangazwa hivi karibuni na kituo cha televisheni cha CNN  na kuonyesha jinsi vijana wa kiafrika walivyokuwa wakiuzwa kama watumwa katika masoko ya mnada nchini Libya. 
Akizungumza kuhusu kisa hicho cha karaha, kansela Angela Merkel amesema:"Mada ya uhamaji kinyume na sheria inakamata nafasi muhimu katika bara lote la Afrika wakati huu tulio nao kwasabau kuna rirpoti zinazosema vijana wa kiafrika wamekuwa wakiuzwa kama watumwa nchini Libya. 
Na hiyo ndio sababu mada hiyo inazusha jazba kubwa katika mkutano huu. Kwa hivyo yameibuka masilahi ya pamoja ya kukomesha uhamaji kinyume na sheria na kuwafungulia njia watu kutoka Afrika kuweza kuja Ulaya kusoma au kujifunza kazi."
TAG