
Halmashauri
ya Ushetu wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, imeanzisha
kilimo cha Korosho ili kutekeleza azima ya serikali ya kuwa na mazao mkakati.
Mkurugenzi Mtendaji
Michael Matomola amesema hayo
katika uzinduzi wa kilimo cha zao hilo uliofanyika katika ofisi za Halmashauri
hiyo.
Amesema
wamedhamiria kutii wito wa serikali kupitia agizo lililotolewa na Waziri
Mkuu Kasimu Majaliwa la kuwa na mazao mkakati, ambapo wameamua kulima
korosho kutokana na mazingira ya eneo
hilo.
Fortunus Kapinga
ni Mtafiti wa korosho kanda ya Kusini ambapo amekili eneo hilo
linafaa kwa kilimo hicho huku
akibainisha mahitaji yanayotakiwa ili kustawi vizuri.
Anna Ngongi na Paul Senni ni Maafisa kilimo
wa Halmashauri hiyo wamesema wakulima wameitikia kilimo hicho kupitia uhamashaji uliofanywa na
viongozi wao wakiwemo Madiwani.
Halmashauri ya
Ushetu mpaka sasa imepokea kiasi cha kilo 80 za mbegu kutoka bodi ya korosho Tanzania, na kuzisambaza kwa kata
ya Mapamba na Nyamilangano hu kukiwa bado kuna uhitaji
kwa maeneo mengine.
No comments
Post a Comment