Imeelezwa kuwa tabia ya kuwajengea uwezo watoto katika kutunza mazingira,ni moja kati ya hazina kubwa kwa taifa itakayo saidia kutunza uoto wa asili .
Hayo yamebainishwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Kahama B CONRAD NKUBA,iliyopo
halmashauri ya mji wa Kahama wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wakati
akizungumza na Baloha fm ofsini kwake.
Amesema kwa kulitambua hilo shule hiyo imekuwa
ikiwafundisha watoto hao suala la mazingira kikamilifu ikiwa ni pamoja na
kupanda miti mbali mbali ili kuboresha mazingira ya shule.
Aidha amesema shule hiyo tayari imepokea miti 140 ya
matunda aina ya miembe kutoka halmashauri ili kuweza kupanda na kuongeza kuwa
kufikia mwaka 2018 shule hiyo itahakikisha inaweka uzio wa miti itakayo pandwa
kuzunguka shule ili kuepuka uvamizi wa watu.
Nkuba ameongeza kuwa shule
hiyo ya Kahama B mbali na kupokea miti pia imekuwa na utaratibu wa kununua miti
aina ya midodoma kila mwezi ili kuboresha mazingira ya shule na kupata kivuli
kwa wanafunzi .
No comments
Post a Comment