
Umoja wa Mama Lishe katika hospitali ya
wilaya ya Kahama ,mkoani Shinyanga wameandamana mpaka kituo cha Polisi Kitengo
cha Dawati la Jinsia Kahama kupinga kitendo cha Mama Lishe mwenzao anayedaiwa kumfanyia ukatili wa kumpiga
kichwani mtoto wa binamu yake na
kumsababishia majeraha.
Wakizungumza na Baloha FM baadhi ya Mama Lishe hao wamemtaja mama huyo
kuwa ni Veronica Ugwang'a mwenye
umri wa miaka (40)
anadaiwa kumpiga mtoto mwenye umri wa miaka (9)
jina limehifadhiwa
Kwa upande wake Mwanamke huyo aliyefanya ukatili huo alipohojiwa amekiri kutenda ukatili huo kwa madai kuwa mtoto huyo amekuwa akijisaidia kitandani mara kwa mara.
Naye Afisa Kitengo cha Dawati la Jinsia
wilayani Kahama Coplo.Methusela Gumba
ameelezea kuhusiana na tukio hilo huku akiwataka watu kutoa ushirikiano ili
kufichua ukatili katika jamii.
Kitendo hicho cha kikatili kinatajwa
kufanyika katika mfululizo wa siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia
maadhimisho ambayo hufanyika Novemba 25
mpaka Disemba 10 ya kila mwaka.
No comments
Post a Comment