
Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani Shinyanga imeagizwa kuhamia eneo la Ntobo kabla ya Juni 30 ,mwaka 2018.
Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri wa
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Joseph George Kakunda
katika hafla ya makabidhiano ya majengo yaliyokuwa yanatumiwa na halmashauri ya Ushetu
na kuyakabidhiwa halmashauri ya mji wa Kahama baada ya Halmashauri hiyo ya Ushetu kujenga majengo yao eneo la Nyamilangano.
Naibu waziri huyo wa TAMISEMI amesema
kuwa mabishano ya kuamua makao makuu ya
halmashauri ya Msalala serikali haihusiki hivyo ni
matatizo ya ndani ya halmashauri hiyo.
Aidha Naibu waziri huyo amesema kuwa
tamko hilo litatolewa kwenye maandiko ndani ya siku 10 huku akiitaka
halmashauri hiyo kubeba jukumu la kuhamia
Ntobo.
Imeelezwa kuwa Halmashauri ya Msalala imechelewa kuhamisha ofisi zake katika eneo lake baada ya kuwepo
mgongano wapi makao makuu ya halmashauri hiyo yawekwe kati ya Segese na Ntobo
na hatimaye wamekubaliana makao makuu kuwa eneo la Ntobo.
No comments
Post a Comment