Wananchi wilayani kahama wametakiwa kupanda miti kwa kuzitumia mvua zinazoendelea kunyesha ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kauli hiyo
imetolewa na baadhi ya wananchi mjini kahama wakati wakizungumza na baloha fm
kuhusu kampeni ya upandaji wa miti iliyoanzishwa mkoani humo ya shinyanga mpya
mti kwanza.
Wamesema licha
ya mvua zinazoendelea kunyesha wananchi hawana destri ya kupanda miti ingawa
serikali imekuwa ikihimiza wananchi wote kupanda miti hiyo.
Kwa upande
wake meneja msaidizi wa wakala wa misitu Tanzania wilaya ya kahama MOHAMED DOSA amewataka wananchi kupanda
miti kwa kuwa kuna mabadiliko makubwa yaliyotokana na kutoweka kwa miti.
Hata hivyo
amesema mpaka sasa taasisi hiyo ya wakala wa misitu kahama imeotesha miti laki
tano kwa ajali ya kupandwa katika maeneo mbalimbali ya mji wa kahama katika
taasisi za umma.
No comments
Post a Comment