Mwenyekiti wa Umoja
huo wilaya ya KAHAMA, AGUSTINO MALYA amesema hayo wakati akizungumza na BALOHA
FM.
MALYA amesema wameamua kuunda umoja huo ambao utatambulika kwa
jina la Golden city Arts unity lengo likiwa ni kusaidiana wao kama vijana
pamoja na kuendeleza na kukuza sanaa ya muziki ndani na nje ya KAHAMA.
Aidha Ameongeza
kuwa wamelenga kufikisha ujumbe katika jamii kupitia sanaa ya muziki ikiwemo
kupinga mauaji ya vikongwe na watu wenye Ualbino na mambo mengine yanayoenda kinyume
na maadili ya Kitanzania
Kwa upande wao,
baadhi ya wasanii ambao wameshiriki kuunda umoja huo wamesema utawasaidia
kufikia malengo yao kwani sanaa ni kazi kama kazi zingine.
Kadhalika wamewataka
wazazi wenye watoto ambao wanavipaji kuwapa uhuru wa kufanya sanaa.
No comments
Post a Comment