
Kocha wa Real Madrid
Zinedine Zidane amesema Mshambuliaji wa timu hiyo, Gareth Bale amepona na yuko
fiti kurejea uwanjani.
Bale atacheza kwa mara ya
kwanza leo baada ya kukaa nje kwa miezi miwili.
Kocha Zidane amesema madaktari
wamethibitisha kuwa Bale amepona na yupo tayari kukabili wapinzani wao katika
michuano mbalimbali inayoshiriki timu hiyo.
Amefafanua kuwa
Mshambuliaji huyo ataongeza nguvu katika kikosi cha Real Madrid.
Bale amekuwa nje ya dimba
baada ya kupata na majeraha ya goti na baadae nyonga na kwa sasa amejumuishwa
katika timu itakayocheza na Fuenlebrada kwenye kombe la Copa del Rey.
Bale raia wa Wales
alionekana mara ya mwisho uwanjani walipoichapa Borussia Dortmund 3-1 kwenye
kombe la klabu bingwa Ulaya.
Amefunga jumla ya magoli 70 katika michezo 159 aliyoichezea Real Madrid.
No comments
Post a Comment