Ukosefu wa
vyoo katika shule ya msingi kahama A
wilayani kahama mkoani shinyanga umesababisha wanafunzi wa shule hiyo kutumia
vyoo vya shule ya jirani Kahama B.
Akizungumza na
baloha fm diwani wa kata ya kahama mjini Hamidu Kapama amesema kuwa choo cha awali kimetitia na hivyo kubomoka hali
inayoweza kusababisha milipuko ya magonjwa hasa kipindi hiki cha masika.
Amesema kuwa
baada ya tukio hilo ameweza kuitisha
mkutano na wazazi lengo ikiwa ni kuchangia ujenzi wa vyoo bora katika shule
hiyo.
Kutokana na kikao hicho wazazi na walezi wameonyesha ushiriki mzuri kwa
kuahii kuunga juhudi za Rais Magufuli kwa kuahidi kuchangi mifuko ya saruji.
Aidhaa amesema
kuwa lengo lao ni kujenga choo chenye matundu 12 ili wanafunzi waweze kupata mahali pa
kujisitiri na tathimini ya ujenzi huo inatarajia kughalimu zaidi ya shilingi
milioni 10.
No comments
Post a Comment