Imeelezwa kuwa chanzo cha kupata matokeo mabaya ya ufaulu, baadhi ya shule za msingi na Sekondari katika halmashauri ya Msalala mkaoni Shinyanga, ni kutokana na wanafunzi na walimu kutumia muda mwingi kutafuata maji kwaajili ya matumzi ya shule.
Akizungumza leo katika kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo, Diwani wa Kata ya MWANASE, SAMSON MASANJA amesema shule nyingi hasa zilizo pembezoni zina changamoto ya upatikani wa huduma ya Maji.
Amesema kutokana na hali hiyo, wanafunzi na walimu hulazimika kutumia muda wa asubuhi kufuata maji umbali mrefu kwaajili ya matumizi ya shule hivyo kuathiri ratiba ya masomo darasani.
Masanja ameshauri Halmashauri hiyo kuja na mapango kabambe wa kukabiliana na hali hiyo ili kuwawezesha wanafunzi kufaulu mitihani yao.
Awali halmashauri hiyo imeeleza kua sababu zilizosababisha halmashauri hiyo kupata matokeo mabaya kwa shule za Msingi na Sekondari ni kutokana na ukosefu wa Chakula Mashuleni, Utoro, ukosefu wa walimu hasa wa masomu ya sayansi pamoja na mwamko duni wa wawazi.
Aidha halmashauri hiyo kupitia Kitengo cha Elimu imesema imejipanga kuinua kiwango cha ufaulu mwaka huu.
Na Michael Francis Bundala.
No comments
Post a Comment