WIZARA ya Ardhi Maendeleo ya Makazi imetangaza kulipiga
mnada jengo la klabu ya Yanga, makao makuu makutano ya mitano ya Twiga na
Jangwani, Dar es Salaam kesho.
Katika tangazo lililotoka leo, Wizara ya Ardhi imesema
hatua hiyo inafuatia kesi iliyofunguliwa na Kamishna wa Ardhi katika Baraza la
Ardhi na Nyumba Wilaya na Temeke na Ilala dhidi ya Yanga.
Na kwa mujibu wa tangazo la kampuni ya udalali ya
Msolopa Investmenst Limited, Dalili Maurid Msolopa amesema mnada huo utafanyika
hapo baadaye hapo hapo Jangwani, baada ya kushindikana hii leo.
Akizungumzia hilo, Katibu Mkuu wa Yanga, Charles
Boniface Mkwasa amesema kwamba ameshitushwa na tangazo hilo kwa kuwa tayari
wapo katika jitihada za kulipa madeni yao.
Mkwasa
amesema kupitia utaratibu ambao wamejiwekea
wanaamini utakuwa msaada wa kumaliza kulipia deni hilo.
Katika hatua nyingine Mkwasa amesikitishwa na kuwepo kwa
hali hii wakati timu ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa ngao ya Jamii shidi
ya mahasimu wao Simba.

No comments
Post a Comment