KUKOSA ELIMU YA AFYA YA UZAZI NI CHANZO CHA MIMBA KATIKA UMRI MDOGO.

Imeelezwa  kuwa   mtoto wa kike  aliye  chini ya umri wa miaka 20 akibeba  mimba  ana  kidokezo cha hatari  kiafya hivyo anatakiwa kujifungulia  hospitali .

Hayo yamebainishwa leo  na Daktari  Frola Mwinuka kutoka Halmashauri ya Mji  Kahama, wakati  akiongea kwenye kipindi cha Darubini Halisi kinachorushwa na Baloha Fm.


Amesema ni vyema  kujifungulia katika vituo vya afya ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza wakati wa kujifunga  ikiwamo kupoteza maisha  Mama na Mtoto anayezaliwa.



Aidha mesema takwimu za mwaka 2015 zinaonyesha kuwa wasichana mililoni 14 wanabeba  mimba kila mwaka Duniani,  huku Mkoa wa Shinyanga ukitajwa kuongoza  nchini Tanzania ukifuatiwa na Mkoa wa Tabora.

Amesema  chanzo ha mimba za utotoni ni umaskini katika familia, kukosa elimu ya afya uzazi, anasa, pamoja na ndoa za utotoni na kwamba mschana anayepata mimba chini ya umri huo anaweza akaathirika kimwili na za kisaikolojia.

Hata hivyo amesema  ili kunusuru hali hiyo sheria ichukue mkondo wake kwa wale watakaokuwa visababishi, pia jamii ihamasishe wanawake wenye mimba kwenda  kujifungulia hospitalini.


Na Mary Clemency       Baloha fm.
TAG