AZAM FC: MSIWE NA WASIWASI KUHUSU MBARAKA YUSSUF, NI MALI YETU.


UONGOZI wa Azam FC umewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuhusu usajili wa mshambuliaji Mbaraka Yussuf, aliyewekewa pingamizi na timu yake ya zamani ya Kagera Sugar.

Azam FC imefanikiwa kumsajili Mchezaji huyo Bora Chipukizi wa VPL msimu uliopita kwenye usajili huu, kwa mkataba wa miaka miwili na tayari ameungana na kikosi hicho kilichomaliza kambi yake ya siku 10 nchini Uganda juzi kujiandaa na msimu ujao.


Kagera Sugar inadai bado ina mkataba na mchezaji huyo wa miaka mitatu, ikipeleka pingamizi hilo la usajili kwenye Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ambayo inatarajia kukutana Jumapili hii kupitisha usajili.


Taarifa iliyotolewa na Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, leo imeeleza kuwa timu hiyo ilimsajili mchezaji huyo kwa kufuata taratibu zote za usajili, huku akidokeza kuwa tayari Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) limeidhinisha usajili wake kupitia mfumo mpya wa usajili wa kimtandao wa TMS.


Wakati huo huo, Kiungo Kinda Joseph Kimwaga baada ya miaka kadhaa toka aondoke akaenda kucheza soka katika club ya Simba SC na baadae Mwadui FC ya Shinyanga , amezungumzia kurejea kwake Azam Fc.
Kimwaga pia akawazungumzi wachezaji waliokuwepo Azama Fc na sasa wameondoka na kujiunga na vilabu vingine na kusema kuwa itakuwa ngumu kuzoeana nao lakini anaamini itawezekana kuzoeana kwa muda mfupi.


Na Dira ya Michezo Team,

                                                             Baloha fm.



TAG