Mashetani Wekundu walilazimika kusubiri hadi dakika ya 70 kupata goli la kwanza katika uwanja wa Old Trafford baada ya kubanwa vizuri na Leicester.
Rashford ndiye mchezaji aliyekwamisha wavuni bao la kwanza baada ya Romelu Lukaku kukosa penalti, wakati Marouane Fellaini akiweka kimiani bao la pili.
Akizungumza na BT Sport baada ya mechi, Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza amekiri kuwa anafurahia kubeba uzito wa timu kwa kufunga goli muhimu kwa United.
"Tulitengeneza nafasi nyingin sana kipindi cha kwanza na ilionekana kama tungeshinda kama zile siku za nyuma," alisema. "Lakini timu iliendelea vema na jukumu na nashukuru tulipata goli. Ninapopata nafasi, najiamini nitafunga magoli."
United waliendelea kushinda bila kuruhusu goli katika mechi zao tatu za mwazo Ligi Kuu Uingereza kwa mara ya sita katika historia.

No comments
Post a Comment