NKURLU AAMURU KUNYANG'ANYWA WATAKAOZOROTESHA MRADI WA ADP BUSANGI, KAHAMA.


Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkulu amesema wananchi watakaoshindwa kuendeleza miradi mbalilbali ya maendeleo inayoachwa na mashirika mbalimbali baada ya kumaliza muda wake ikiwamo mradi wa ADP  BUSANGI katika Halmashauri ya Msalala.

Ameyasema hayo wakati wa makabidhiano ya mradi wa maendeleo ya jamii wa ADP Busangi  katika kata ya Ntobo uliokuwa ukitekelezwa na shirika la World Vision Tanzania kwa kuishirikisha wananchi.


Nkurlu amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala kuwanyang'anya miradi huo endapo wananchi watakalia malumbano na kushindwa kufanya shughuli za maendeleo na kuwapatia wananchi wengine wa halmashauri hiyo.

Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Msalala Simon Berege amelipongeza shirika hilo kwa kutekeleza mrdai huo kwa muda mrefu na hivyo kuleta maendeleo kwa wananchi wa halmashauri hiyo.
TAG