ENDUIMENT WAISAIDIA SH. MILL 99 VIJIJI 11 LONGIDO.
Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori ya Enduimet (WMA) imekabidhi Shilingi Milioni 99 kwa vijiji 11 wilayani Longido kwa ajili ya shughuli za maendeleo ya wananchi.
Fedha hizo zimetolewa na kampuni ya uwindaji ya Shangri-la iliyopo wilayani Longido mkoani Arusha.
Imeelezwa kuwa fedha hizo zinatokana na mapato yaliyokusanywa kwa ajili ya shughuli za uwindaji katika kampuni hiyo.
Vijiji hivyo 11 vinavyounda jumuiya hiyo kwa kutoa maeneo ya shughuli za uwindaji kila kimoja kimepewa Shilingi milioni 9.
Mkuu wa Wilaya ya Longido, Daniel Chongolo amewaagiza watendaji wa vijiji husika kuhakikisha wanaainisha mapato na matumizi ya fedha hizo katika kila kijiji ili zijulikane zilivyotumika.
Chongolo amesema kumekuwepo na ubadhirifu wa fedha za wananchi unaofanywa na baadhi ya watendaji wanaojali masilahi binafsi ikiwemo kujilipa posho.

No comments
Post a Comment