DONE DEAL: OSMAN DEMBELE RASMI BARCELONA, KILICHOBAKI NI KUMALIIZANA TU.

 
 
Mfaransa, Ousmane Dembele anatarajiwa kutua Barcelona Jumapili na Jumatatu atafanyiwa vipimo kabla ya kusaini mkataba wa miaka mitano Camp Nou.
 
Bosi wa Barcelona Ernesto Valverde amesema kuwa Ousmane Dembele ataleta mafanikio kwa miamba hao wa Catalan.

Ilitangazwa Ijumaa mchana kuwa Barcelona walikuwa wameshafikia makubaliano ya dili la paundi milioni 96.8 na Borussia Dortmund kwa ajili ya uhamisho wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa mchezaji ghali zaidi wa pili duniani.

Mshambuliaji huyo amefunga mara 10 na kutoa pasi za mabao 18 katika mechi 47 alizocheza Dortmund msimu wa 2016-17, na Valverde amebainisha kuwa uzalendo unamshinda kuendelea kusubiri mchezaji huyo kutua Camp Nou.

"Yeye [Dembele] ni mchezaji anayetuhakikishia uthabiti. Tumepoteza kitu kwa hakika," Valverde aliwaambia waaandishi. "Anaweza kucheza pande zote na anaweza kutupatia nafasi nyingi katika mashambulizi. Ana kasi, weledi na ufundi. Tunatumai atatuletea vitu adimu."

Valverde, pia amedokeza kuwa biashara ya uhamisho ya Barcelona haijakamilika bado msimu huu.
"Bado tunasubiri. Tuna muda wa kutosha hadi dirisha la usajili litakapofungwa," bosi huyo wa Barcelona aliongeza.

Barcelona wataendelea na kampeni za La Liga 2017-18 kwa ziara kwenda Alaves Jumamosi usiku.

Lakini pia dembele anaungana na Moussa Sissoko na Termoe  Bakayoko kutemwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa katika kiikosi kilichoitwa wiki hii kwa ajili ya kutekeleza miichezo ya kalenda ya wiki ya FIFA.
TAG