WORLD VISION YAKABIDHI MRADI WA BUSANGI ADP-KAHAMA.
Shirika la WORLD VISION Tanzania leo limekabidhi mradi wa BUSANGI ADP kwa jamii ya tarafa ya Msalala ambao utakuwa unasimamiwa chini ya serikali ya Wilaya ya Kahama.
Katika Risala iliyosomwa na MWENYEKITI WA COMMUNITY DEVELOPMENT (CDO) PETER MSHENGE amesema mradi huo umeendeshwa na World Vision Tanzania kwa miaka 17 hadi kukabidhiwa kwa wananchi na serikali.
Aidha Mradi wa Busangi ADP ulipo katika Kijiji cha Busangi umewanufaisha wananchi wa Tarafa ya Msalala katika sekta mbalimbali ikiwamo sekta ya Kilimo, Elimu na Afya.
Kwa uapnde wake Mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu amesema serikali imeanzisha shirika la jamii la MSALALA COMMUNITY DEVELOPMENT (CDO) ambalo litasaidia kuunganisha nguvu za wananchi wanaonufaika na mradi huo.
Baadhi ya wananchi walionufaika na mradi huo John herman na Adriano Michael wamepolipongeza Shirika la World Vision Tanzania na kwamba mradi huo utakuwa na manufaa kwa wananchi wa Tarafa ya Msalala na halmashauri kwa ujumla.
Na Alfred bulahya. Baloha FM, Kahama.

No comments
Post a Comment