MWIGULU; ASIYEVAA KOFIA NGUMU SHINYANGA AWEKWE NDANI.



Waziri wa mambo ya ndani ya nchi  Mwigulu  Chemba ameliagiza Jeshi la polisi  Mkoani  Shinyanga  kuwachukulia hatua madereva pikipiki na abiria  ambao hawavai  kofia ngumu.

Akiwa ziarani  Mkoani   Shinyanga  hivi karibuni  Waziri  Nchemba  amesema   kuna baadhi ya abiria wanakataa kuvaa kofia ngumu  kwakudai kuwa wanaharibu  nywele zao  hali ambayo  inahatarisha usalama wao.

Aidha amesema  Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani  kinatakiwa  kuwachukulia hatua kali  wale watakaobainika   kukiuka  sheria ya  usalama barabarani.

Nao baadhi ya wananchi  wa  wilaya  ya  Kahama Emmanuel Sosoma,Sali Bunzali na Robert Misungwi  kupitia kipindi cha Darubini Halisi cha Baloha Fm  wamepongeza  agizo  hilo  lililotolewa na serikali   kwakutoa mitazamo yao tofauti.

Na Mary Clemence    Baloha FM     Kahama.
TAG