DEMBELE APIMA AFYA JUMATATU HII.

Mfaransa Ousmane Dembele amepiga hatua kuwa mchezaji wa Barcelona baada ya kumaliza vipimo vya afya Jumatatu. 
 
Ousmane Dembele amefanyiwa vipimo vya afya kuelekea uhamisho wake kujiunga na Barcelona.

Borussia Dortmund wamekubali kumuuza Dembele kwa miamba hao wa La Liga kwa malipo ya awali ya euro milioni 105  Ijumaa iliyopita na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 atasaini mkataba wa miaka mitano Jumatatu kama sehemu ya kutangazwa rasmi kama mchezaji wa Barcelona.

Kwanza, utaratibu wa vipimo ulihitaji kufanywa na Barca walichapisha kwenye akaunti yao ya twitter video ya Dembele akiwasili Hospitali ya Barcelona.

"Dembele amekamilisha vipimo na sasa anaelekea kwenye kituo cha afya cha Barcelona Ciutat Esportiva Joan Gamper," klabu hiyo imechapisha kwenye tovuti yao baada ya tukio hilo. 

Mchezaji huyo wa zamani wa Rennes atavaa jezi namba 11 Camp Nou, ambayo iliachwa na Neymar aliyetimkia Paris Saint-Germain.
TAG