HIZI NDIZO DONDOO ZILIZOMFANYA OKWI KUWA MCHEZAJI BORA WA WIKI VPL.

 
Emmanuel Okwi ameandika historia ya kuwa mchezaji wa kwanza mwenye magoli mengi katika ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa kuweza kufunga magoli 4.
 
Kiungo mshambuliaj wa Simba raia wa Uganda, Emmanuel Okwi ameibuka mchezaji bora wa wiki baada ya kuwa kwenye kiwango bora wikendi iliyopita. 

Emmanuel Okwi amefanikiwa kuibuka nyota wa wiki baada ya  kufanikiwa kufunga magoli manne kwenye ushindi wa goli saba kwa bila dhidi ya RUVU Shooring siku ya Jumamosi.
 
Mganda huyo ambaye aliwapa wakati mgumu mabeki wa RUVU,  alitumia dakika 53 tu kufunga magoli yote manne (18, 22, 35, 53) katika mchezo huo huku magoli mengine yakifunga na Shiza Kichuya, Juma Luizio na Erasto Nyoni.

Pia Okwi anaungana na mchezaji mwingine wa simba, Juuko Mursheed kujiunga na timu ya taifa baada ya kutajwa tena na kocha wa muda wa timu hiyo ya taifa ya Uganda, Uganda Cranes Mosses Basena ambapo ni miongoni mwa wachezaji zaidi ya 25 waliotajwa kuingia kambini kwa ajili ya michezo ya kufuzu kombe la dunia 2018 Russia.

Pazia la Ligi Kuu Bara lilifunguliwa wikendi iliyopita, katika hatua nyingine Ligi itarejea tena wiki mbili zijazo baada ya kupisha mechi za timu ya Taifa.
TAG