Kituo cha Sheria na
Haki za Binadamu (LHRC), kimemtaka Kaimu Jaji Mkuu, Ibrahim Juma kukemea
hadharani shambulizi lililofanyika katika ofisi za wanasheria za Immma Advocates.
Mkurugenzi wa LHRC,
Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema tangu kutokea mlipuko usiku wa kuamkia Agosti
26, hakuna kiongozi wa Serikali ambaye amekemea.
Amesema hata kaimu
jaji mkuu anayesimamia mhimili wa Mahakama naye amekaa kimya kama vile hakuna
tukio lililotokea.
Dk Kijo-Bisimba
amesema leo Agosti 29 kuwa, kitendo cha mawakili kuvamiwa kimewatia hofu
wanataaluma hao.
Katika hatua nyingine Rais wa Chama cha
Wanasheria Tanganyika ‘TLS’, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu
ameendelea kulaani tukio la kuvamiwa ofisi za Wanasheria IMMMA Advocates na
kusema ni muhimu jambo hilo likapigiwa kelele kwa kuwa siyo la kisiasa.
Lisu amesema hayo
baada ya kualikwa katika mkutano wa kituo cha Sheria na Haki za Binadamu
(LHRC)na kusema kuna mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali ndani ya Tanzania
ambayo yanafanya kazi za kutetea haki za binadamu lakini wengi wao katika tukio
hili wamekuwa wapo kimya.
2.Waziri wa Mambo
ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Dk Augustine
Mahiga amesema kikundi chochote cha kigaidi au kiharamia kitakachoingia katika
moja ya nchi zilizo katika ukanda wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika
(Sadc) kitajuta.
Akizungumza kwa sababu kikundi hicho cha uigaidi
kitashambuliwa na majeshi ya nchi zote katika ukanda huo iwapo kitaanza
uchokozi.
Amesema nchi za
Sadc zimeamua kujizatiti katika ulinzi kwa kuunganisha majeshi yake ili
kujiweka sawa na tishio lolote la ugaidi na uharamia zikiamini uchumi wake
hautaimarika kama moja ya nchi itakuwa inasumbuliwa na ugaidi.
Balozi Mahiga
amesema hayo wakati akifunga mazoezi ya pamoja ya kijeshi yaliyopewa jina la
Ex-Matumbawe yaliyoendeshwa na majeshi kutoka nchi saba zilizo katika jumuiya
ya Sadc yaliyofanyika mkoani Tanga na kuhitimishwa jana Agosti 28.
Mkuu wa Majeshi ya
Ulinzi Tanzania (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo, amesema mazoezi ya
Ex-Matumbawe yenye madhumuni ya kimkakati, utendaji kivita na ki-mbinu
yamefanyika nchini kwa mara ya kwanza baada ya kuendeshwa Zambia, Lesotho,
Afrika Kusini, Namibia, Angola na Zimbabwe.
No comments
Post a Comment