Washindi wa
pili wa kome la FA msimu uliopita Mbao FC, leo August 29, 2017 imengia
mkataba wa udhamini kutoka kampuni ya GF Trucks & Equipment LTD.
Msemaji wa Mbao FC, Krisantos Malinzi, ameiambia Goal, udhamini huo utawasaidia katika harakati zao za kuifanya timu hiyo kuendelea kufanya vizuri kwenye michuano ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara na michuano mengine.
“Tunawashukuru GF Trucks & Equipment, kwa upendo wao hadi kuja kutudhamini msaada wao utatusaidia kufanya vizuri kwenye ligi na kuweza kutimiza malengo yao ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara,”amesema Malinzi.
Mkataba uliosainiwa una thamani ya Tsh. 140 milioni ambapo ndani ya kiasi hicho kampuni ya GF Trucks & Equipment itatoa basi la kusafiria wachezaji lenye thamani ya shilingi milioni 70 huku kiasi kingine cha shilingi milioni 70 wakipewa kwa ajili ya matumizi mengine.
Basi na jezi za Mbao FC vitakuwa branded na GF Trucks & Equipment, udhamini huo ni wa mwaka mmoja lakini basi ambalo litakuwa branded na GF Trucks & Equipment litakaa na nembo ya wadhamini kwa miaka miwili.
GF Trucks & Equipment wanakuwa wadhamini wapili rasmi wanaoidhamini Mbao FC wakiungana na kampuni ya utengenezaji wa maziwa ya Cowbell.

No comments
Post a Comment