Arsene Wenger amekataa kwa jeuri amekataa kumuuza mchezaji wa kimataifa wa Chile majira ya joto, lakini mazungumzo yameanza na Man City.
Alexis Sanchez ana shauku kubwa kujiunga na Man City na Washika Mtutu sasa wanafikiria kukubali kumuuza mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile, baada ya kukataa ofa kadhaa kipindi chote cha majira ya joto.
Raheem Sterling ni miongoni mwa machaguzi ambayo yametajwa katika mazungumzo baina ya klabu hizo mbili saa 48 zilizopita, ingawa Goal inaelewa kuwa ni Arsenal walioshinikiza mchezaji huyo kuwa sehemu ya dili.
Fabian Delph pia ametajwa na City mahasimu wao wa Ligi ya Uingereza wanapotaka kufanya makubaliano ambayo yatazidaidisha pande zote mbili kabla ya dirisha la uhamisho kufungwa Alhamisi.
Kwa sababu hata hivyo Alexis alishafikia makubaliano na City, Arsenal watakuwa na kazi rahisi kufikia makubaliano kwa dau lolote watakaloona lina faida kwao.
Uongozi wa City unaamini mchakato wa usajili utamalizika kabla ya Alhamisi na pia wanaimani kubwa ya kumpata Jonny Evans kutoka West Brom licha ya kutajwa kwenye tetesi za kuingia kwenye rada za Arsenal pia.
Mshambuliaji huyo wa Arsenal aliwaambia wachezaji wenzake wa Chile mwishoni mwa msimu uliopita kuwa anatamani kuungana na Guardiola, ambaye walishawahi kufanya wote kazi Barcelona na pia amefikia makubaliano ya masharti binafsi na Blues majira ya joto.
Baada ya michuano ya Kombe la Shirikisho, ambapo aliweka bayana kuwa ameshafanya maamuzi juu ya mustakabali wake, aliitaarifu Arsenal kuwa anataka kutua Etihad na asingependa kusaini mkataba mpya na miamba hao wa London.
Vyanzo ambavyo vipo karibu na City vimeshangazwa na kitendo cha Arsene Wenger kukataa dili tangu Julai hadi Agosti, ingawa kumekuwa na pendekezo kuwa Mfaransa huyo alikuwa tu akichelewesha jambo ambalo hawezi kuliepuka, na amenyima Pep Guardiola fursa ya kumtumia Sanchez mechi za awali ufunguzi wa Ligi Kuu.
City na Arsenal hatimaye zimeshaanza mazungumzo tangu wikiendi na ingawa msemaji wa Gunners amesema kwamba ofa rasmi bado haijatolewa, Blues wanatarajiwa kukamilisha dili hilo haraka, licha ya kuwa Alexis ameshatua Chile akijandaa kwa mechi ya kufuzu Kombe la dunia dhidi ya Paraguay na Bolivia.
Inasemekana aliomba ruhusa kwa ajili ya maandalizi ya mechi ya Alhamisi, na vyanzo vilivyo karibu na mchezaji huyo vimesema kuwa mchezaji huyo anaamini atarejea Uingereza akiwa mchezaji wa Man City siku zijazo.
No comments
Post a Comment