Manchester
United imekuwa timu ya Kwanza kupata ushindi katika uwanja wa Emirates tangu
mwezi Januaru mwaka huu baada ya jana usiku kuinyuka Arsenal bao 3-1.
Manchester
United walipata bao la kwanza katika dakika ya 4 ya mchezo lililofungwa na Antonio
Valencia na kuiweka kifua mbele timu yake kabla ya Jesse Lingard kufunga la
pili dakika ya 11 baada ya kumkoonya mpira Shkodran Mustafi.
Kikosi
cha Jose Mourinho kilipunguzwa na kuwa na wachezaji 10 katika dakika za mwisho
baada ya Paul Pogba kupewa kadi nyekundu kwa kucheza rafu.
Kabla
ya Pogba kupewa kadi nyekundi alimshinda nguvu Koscielny na kumpatia pasi
Lingaard ambaye alifunga bao la tatu dakika ya 63 na kuipatia United ushindi
huo.
Bao
la kufutia machozi la Arsenal lilifungwa na Alexandre Lacazette katika dakika
ya 49
Kipa
wa United, David de Gea ameisaidia timu yake katika mechi yote.
Katika
michezo mingine iliyofanyika jana Chelsea ikiwa nyumbani imeiadhibu Newcastle
United bao 3-1, wakati Brighton ikipokea kichapo cha bao 5-1 kutoka kwa Liverpool.
Nayo
Everton imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani baada ya kushinda bao 2-0
dhidi ya Huddersfield huku Leicester ikipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi
ya Burnley.
Michezo
mingine Stoke 2 Swansea 1, Watford 1 Tottenham 1, West Brom 0 Crystal Palace 0.
No comments
Post a Comment