UNESCO YATOA MSAADA KWA VYOMBO VYA HABARI NCHINI.



SHIRIKA la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) limekabidhi vifaa vya radio kwa radio za jamii nne vyenye thamani ya mamilioni ya shilingi.

Unesco imesema kwamba utoaji wa vifaa hivyo umelenga kuongeza usikivu wa mawimbi ya radio katika maeneo ya vijijini.

Shughuli ya kukabidhiana imefanyika Agosti 17 mwaka huu.

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Zulmira Rodrigues amesema kwamba UNESCO inatambua kazi nzuri zinazofanywa na radio hizo za jamii za kuwafikia wananchi wengi zaidi.

Aidha amesema ni muhimu  kwa radio hizo za jamii kujiangalia na kujitunza zenyewe ili wasiingie katika matata na kuchapisha au kutangaza habari baada ya kukamilika kwake.

Meneja  wa radio ya Jamii ya Baloha FM, Samada Maduhu ameishukuru UNESCO kwa kusaidia kituo chake na kwamba wanatarajia kufikia wilaya tano.
TAG