AUBAMEYANG ASIMAMA MWENYEWE TUZO ZA AFRIKA.
Shirikisho la soka ulimwenguni FIFA jana ilitangaza orodha ya majina ya wachezaji 24 wanaowania tuzo la mchezaji bora wa FIFA kwa mwaka 2017.
Shirikisho hilo la kandanda duniani ilitoa orodha hiyo huku ikibainika kuwa klabu ya Real Madrid ya Uispania ndio imeingiza majina ya wachezaji wengi zaidi.
Wachezaji saba wa Real Madrid wamepata nafasi ya kuingia katika orodha hiyo, ambayo mchezaji mmoja pekee wa Afrika amefanikiwa kuteuliwa.
Pierre Emerick Aubameyang ambaye ni nahodha wa timu ya taifa ya Gabon anayechezea Borussia Dortmund ya Ujerumani ndiye mchezaji pekee aliyebahatika.
Baadhi ya wachezaji kutoka ligi ya Primea waliotajwa katika orodha hiyo ni Alexis Sanchez wa Arsenal, Harry Kane wa Totenham Hotspurs, pamoja na Eden Hazard na N'Golo Kante wote kutoka Chelsea.

No comments
Post a Comment