RT YAILILIA SERIKALI ILI KUKUZA RIADHA NCHINI.


Shirikisho la riadha nchini Tanzania (RT) imeomba msaada zaidi kutoka serikalini na mashirika yasiyo ya kiserikali ili kuinua viwango vya michezo hasa katika harakati zake za kutafuta medali zaidi katika mashindano ya kimataifa.

Haya yaliwekwa wazi na katibu mkuu wa shirikisho hilo Wlhelm Gidabuday, wakati wa sherehe za kualika nyumbani timu ya riadha iliyoshiriki mashindano ya dunia yaliyokamilika wikendi iliyopita Jijini London ambapo Tanzania ilijishindia medali moja.


Gidabuday alisema kushinda medali moja ni sawa na kupanda mbegu mmoja kwenye ardhi yenye rotuba kwani uwezekano wa mbegu hiyo kukua na kuzaa matunda uko juu.


Kulingana naye medali ya shaba iliyoshindwa na Tanzania jijini London itazaa medali nyingi zaidi mradi tu nchi hiyo itazidi kushiriki mashindano mengi. Kutokana na hilo, katibu huyo mkuu aliomba ufadhili zaidi ili kuwezesha shirikisho hilo kuendesha shughuli zake bila matatizo.



TAG