NDERU, MTAALAM WA SUPER BANTAMWEIGHT AFARIKI DUNIA.


John Nderu ambaye alikuwa bondia katika mizani ya kitaifa ya bantamweight, amefariki dunia. 

Nderu aliyefahamika kwa kuichezea Kenya Prisons miaka ya 70 alifariki akiwa na miaka 75.

Mwanaye Edward Mwaura, alithibitisha kuwa babake alifariki katika hospitali ya Baraka, mjini Nakuru, huku akidokeza kuwa Nderu alikuwa amepata kichaa na kupotea nyumbani siku nane kabla ya kupatikana na kupelekwa kupata matibabu.


Aliyekuwa bingwa wa uzani wa featherweight nchini Kenya, Philip Waruinge, alisema kuwa Nderu alijiunga na ulimwengu wa ndondi nyuma yake walipokutana Madison Square Gardens, Marekani.


Wawili hao walikuwa kwenye kikosi cha Kenya kilichoshiriki mashindano ya jumuia ya madola mwaka wa 1966, jijini Kingston Jamaica ambapo Nderu alishinda medali ya shaba ilihali Waruinge akaibuka na medali ya dhahabu.


Nderu pia aliwakilisha Kenya katika mashindano ya Afrika mwaka 1972 jijini Nairobi aliposhinda medali nyingine ya Shaba.
TAG