MSALALA YAVUKA LENGO KATIKA UKUSANYAJI MAPATO.


Halimashauri ya Msalala Wilayani Kahama imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato baada ya kufanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia mia 1 na 11.

Mwenyekiti wa halimashauri hiyo MIBAKO MABUBU  akizungumza  katika kikao cha kawaida cha baraza la madiwani kilichofika tamati leo amewataka madiwani kutembea kifuambele kwa kuwa wamesaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha ukusanyaji wa mapato.
 

Baada ya kumalizika kwa baraza hilo Mkurugenzi wa halimashauri hiyo SIMON BEREGE amezungumza na Wandishi wa Habari na kusema tayari asilimia 66 ya fedha zilizopatikana zimepelekwa kwenye shughuli za maendeleo.

Na Michael Francis Bundala,   Baloha Fm.
 




TAG