Wananchi wa kijiji cha Butende kata ya Mpunze halmashauri
ya Ushetu wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamemuomba mbuge wa jimbo la Ushetu
bw, Elias Kwandikwa kutatua changamoto ya barabara inayotoka mpunze kuelekea
kijijini hapo ili kurahisisha shughuli za usafirishaji.
Kauli hiyo imetolewa na wananchi hao wakati
wakizungungmza katika mkutano wa hadhara na mbunge huyo alipofanya ziara ya
kutembelea kijiji hicho ili kujionea changamoto mbalimbali zinazowakabili.
Baadhi ya wananchi hao Daud Charles na Hamis Mnyole,
wamesema ubovu wa barabara hiyo umekuwa ni changamoto kubwa ambayo husababisha
madhara kwa watumiaji ikiwemo ajali za mara kwa mara kutokana na magari
kushidwa kupita.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Ushetu Elias
Kwandikwa amesema kuwa serikali kupitia
halmashauri hiyo imekwisha kuanza mikakati ya kutatua changamoto za
barabara na ameahidi kupeleka gari la
kukwangua barabara ili zoezi hilo lianze mara moja.
Aidha Mbunge huyo amewaomba wananchi hao kuendelea kuunga
mkono jitihada za serikali ya awamu ya tano kwani serikali imekwisha wakala wa
barabara TARULA kwa lengo la kushughulikia changamoto za barabara.

No comments
Post a Comment