YANGA YAPINGA KUFUNGIWA KWA BUSWITA.




Klabu ya Young Africans imepinga maamuzi ya kamati ya sheria na hadhi za wachezaji kufuatia maamuzi ya yaliyochukuliwa dhidi ya mchezaji Pius Buswita anaedaiwa kusaini katika klabu hiyo na kwa wapinzani wao wa jadi Wekundu wa Msimbazi Simba.

Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji jana ilitoa taarifa kupitia kwa afisa habari wa TFF Alfred Lucas kuhusu maamuzi iliyoyachukua dhidi ya mchezjai huyo ambaye msimu uliopita aliituikia klabu ya Mbao Fc ya jijini Mwanza.

Akizungumza nasi jijini Dar es salaam mapema hii leo, afisa habari wa Young Africans Dismas Ten amesema mpaka sasa hawajapokea barua yoyote kutoka TFF inayowaarifu maamuzi ya kamati hiyo, lakini wanatambua Buswita ni mchezaji wao halali kutokana na taratibu za usajili walizozitumia.

Hata hivyo Dismas Tena alianza kwa kutoa maneno ya ukali, baada ya kuulizwa kuhusu mchezo wa jana wa Ngao ya Jamii ambao ulishuhudia wakipoteza kwa penati dhidi ya Simba


Hata hivyo TFF kupitia kwa afisa habari wake Alfred Lucas wameendelea na msimamo wa kutambua maamuzi ya kamati na hadhi za wachezaji yaliyotolewa mara baada ya kukutana, na kupitia mapingamizi yaliyowasilishwa mbele yao likiwepo la Buswita.


Wakati huo huo Shirikisho la soka nchini TFF, limewataka radhi wanafamilia wote wa mpira wa miguu kutokana na makosa ya maandishi yaliyoonekana kwenye utambulisho wa Ngao ya Jamii iliyotolewa Jumatano Agosti 23, 2017.

Ngao hiyo ilitolewa mara baada ya mchezo uliokutanisha timu za Simba SC na Yanga SC za Dar es Salaam kwenye Uwanja Mkuu wa Taifa jijini. Katika mchezo huo, Simba ilishinda kwa mikwaju ya penalti 5-4 dhidi ya Yanga na kutwaa Ngao hiyo. 

Afisa habari wa shirikisho la soka nchini TFF Alfred Lucas amesema radhi hizo wamezielekeza kwa Watanzania hususani wanafamilia ya mpira wa miguu popote pale walipo.
TAG