Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa WFP limetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchangisha dola za Marekani milioni 23.6 kuanzia sasa hadi Desemba, ili kukidhi mahitaji ya chakula kwa wakimbizi walioko nchini Tanzania.
Shirika hilo limesema kwamba limelazimika kupunguza mgao wa chakula kwa wakimbizi laki 3.2 kwenye kambi za Mtendeli, Nduta na Nyarugusu, kaskazini magharibi mwa Tanzania kutokana na uhaba wa fedha.
WFP inatoa mahindi, kunde, nafaka, mafuta ya mboga na chumvi kwa wakimbizi ambao wengi wao wanatoka Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments
Post a Comment